Skaut ya Alkafeel imeandaa hema la kuangalia vipaji vya wairaq kwa mara ya kwanza.

Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, imeandaa hema la kuangalia vipaji vya wairaq kwa mara ya kwanza.

Kiongozi wa idara ya ufunzi Sayyid Hussein amesema “Jumuiya imeweka hema la kwanza kwa lengo la kuangalia vipaji, lenye washiriki 75 kutoka mikoa tisa ya Iraq, wamewekwa kwenye makundi matatu, kundi la wahadhiri, maigizo na uimbaji”.

Akaongeza kuwa “Washiriki wanapewa masomo tofauti, kutoka kwa walimu mahiri wenye weledi wa hali ya juu, aidha kuna ratiba ya vipindi vya mapumziko na michezo, vinavyosaidia kupunguza makali ya masomo wanayopewa”.

Akasema kuwa “Jumuiya ya Skaut inajitahidi kufikia malengo yake ya kuandaa hema hili, nayo ni kupata vijana wenye uwezo wa kuanzisha vikundi vya Skaut vipya kwenye miji mingine ya Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: