Muungano wa vyuo vya kiarabu: Chuo kikuu cha Alkafeel kimeweka mazingira mazuri ya kutengeneza kizazi cha wasomi wanaohudumia jamii.

Katibu mkuu wa muungano wa vyuo vikuu vya kiarabu Dokta Amru Izat Salama, amesema kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kinamazingira mazuri ya kutengeneza kizazi cha wasomi wanaohudumia jamii.

Amesema hayo wakati wajumbe wa muungano huo walipotembelea chuo kikuu cha Alkafeel.

Akasema: “Chuo kikuu cha Alkafeel kinamaendeleo makubwa kwenye sekta tofauti, kama vile, maabara, kumbi za madarasa, vifaa vya kufundishia na majengo”, akaongeza kuwa “Mazingira hayo yamekiwezesha kuandaa kizazi cha wasomi wazuri wenye uwezo wa kuhudumia jamii”.

Wageni hao wamepokewa na rais wa chuo Dokta Nusir Muhammad Dahani, na baadhi ya viongozi wa chuo.

Katika kikao wameongea kuhusu njia za kushirikiana na kubadilishana uzowefu, sambamba na kulinda ubora walionao kwa kushirikiana na taasisi zingine zilizopo kwenye muungano huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: