Idhaa ya Alkafeel imehitimisha hafla ya kuadhimisha mwaka wa kumi na tano tangu kuanzishwa kwake.

Idhaa ya Alkafeel chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya idara ya wanawake, imehitimisha hafla ya kuadhimisha mwaka wa kumi na tano toka kuanzishwa kwake.

Kiongozi wa Idhaa bibi Fatuma Mussawi amesema “Idhaa ya Alkafeel imekamilisha maadhimisho ya mwaka wa kumi na tano toka kuanzishwa kwake na imewasha mshumaa wa mwaka wa kumi na sita sambamba na kufanya majlisi iliyopambwa na mashairi pamoja na mambo mengine”.

Akaongeza kuwa “Idhaa ni mfano mwema kwa vyombo vya Habari, inawatangazaji mahiri wenye weledi mkubwa, wanaoandaa na kutangaza mamia ya vipindi vya malezi, Dini na utamaduni”.

Katika hafla hiyo umetolewa muhadhara kuhusu utukufu wa maeneo matakatifu katika Dini, pamoja na misingi ya adabu, imetolewa na bibi Zaharaa Fauzi, sambamba na kugawa zawadi kwa wahadhiri na wadau wa Idhaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: