Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya kinafanya warsha kuhusu usalama wa taarifa na neno la siri katika ulimwengu wa intanet, kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Warsha imesimamiwa na kituo cha mafunzo ya habari na idara ya program za mitandao.
Mkufunzi wa warsha Sayyid Ali Fadhili amesema “Warsha imefanywa kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya wanaofanya kazi kwenye mitandao tofauti ya Ataba, warsha hii inafanywa kufuatia maendeleo makubwa yanayopatikana kwenye sekta hiyo, hivyo watu, mashirika na taasisi mbalimbali zinatakiwa kulinda taarifa zao kwenye mitandao”.
Akaongeza kuwa “Warsha imekuwa na mada nyingi, miongoni mwa mada hizo ni, kutambua usalama wa taarifa na umuhimu wake sambamba na njia kuu zinazotumiwa kulinda taarifa zisidukuliwe au kuibwa, sawasawa ziwe taarifa binafsi au za taasisi”