Mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria.. Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya kuhitimu wanafunzi 4500 wa mradi wa semina za Qur’ani.

Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya kuhitimu wanafunzi (4500) walioshiriki kwenye mradi wa semina za Qur’ani katika mkoa wa Karbala.

Semina hizo zimesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa.

Hafla imefanywa katika eneo la shule za Al-Ameed, mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, wajume wa kamati kuu, marais wa vitengo, viongozi wa hauza na familia za wanafunzi.

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Mustwafa Muwafaq, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi, halafu ukaimbwa wimbo wa taiafa la Iraq na wimbo wa Ataba (Lahnul-Iba).

Ukafuata ujumbe wa Majmaa-Ilmi uliowasilishwa na makamo rais wa Majmaa Dokta Liwaa Abdulhasan Atwiyya, akasisitiza “Umuhimu wa kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu na ulazima wa kukilinda sambamba na kufuata mafundisho yake, hakika kitabu hicho ni muongozo wa Maisha ya watu wa aina zote”.

Akaongeza kuwa “Majmaa-Ilmi kupitia vituo vyake vya Qur’ani hufanya semina za Qur’ani kwa makundi tofauti ya vijana, kwa lengo la kusambaza utamaduni wa kusoma Qur’ani na kufuata mafundisho yake, sambamba na kufundisha usomaji sahihi na kuihifadhi”.

Hafla ilikuwa na vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na ujumbe kutoka kwa wahitimu wa mradi, uliowasilishwa kwa lugha ya kiarabu na kiingereza, igizo lililofanywa na mmoja wa walimu wa mradi akiwa na wanafunzi wanne, wameonyesha baadhi ya masomo yaliyofundishwa kwa weledi mkubwa, usomaji rasmi wa wimbo wa mradi usemao (na kwa Qur’ani tunakuwa hai), waimbaji wa wimbo huo walikuwa washiriki 150.

Majmaa imefanya semina za Qur’ani katika majira ya kiangazi kwenye mikoa kumi na mbili, washiri walikuwa zaidi ya elfu (54), miongoni mwa masomo yaliyofundishwa ni Fiqhi, Aqida, Akhlaq, Sira na Qur’ani, semina zimedumu kwa muda wa siku arubaini na tano, washiriki walikuwa na umri wa miaka 7 hadi 15.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: