Atabatu Abbasiyya imeshiriki kwenye kongamano la kimataifa la Ataba tukufu.

Atabatu Abbasiyya kupitia katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini imeshiriki kweye kongamano la Ataba tukufu katika Atabatu Husseiniyya.

Kongamano limekuwa na mada nyingi, ikiwemo mada ya wajibu wa kuilinda Qur’ani tukufu, kusaidiana, kubadilishana uzowefu, kuongeza mshikamano baina ya Ataba, namna ya kutumia vyombo vya Habari katika kueleza malengo ya Ataba na miradi zake, sambamba na kupitia maazimio ya kongamano lililopita na kuangalia mafanikio.

Aidha kongamano limejadili changamoto mbalimbali zinazoukumba umma wa kiislamu na mbinu za kukabiliana nazo, sambamba na kuimarisha umoja wa taifa na ubinaadamu, kongamano hilo limehusisha Ataba za Iran na Iraq, limefanywa ndani ya jengo tukufu la Atabatu Husseiniyya.

Kongamano limehudhuriwa na makatibu wakuu wa Ataba za Husseiniyya, Abbasiyya, Alawiyya, Kadhimiyya, Askariyya, uongozi wa masjid Kufa, Atabatu Radhawiyya na uongozi wa malalo ya Bibi Maasuma (a.s), kulikuwa na mada za Aqida, utawala, jamii, Akhlaq na Habari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: