Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya mahafali ya wahitimu zaidi ya (2500) wa semina za Qur’ani katika wilaya ya Tuuz-Khurmatu mkoani Swalahu-Dini.
Semina zilisimamiwa na Maahadi ya Qur’ani ya Najafu chini ya Majmaa.
Mkuu wa Maahadi Sayyid Muhandi Almayali amesema: “Kuna umuhimu wa kunufaika na uwezo wa vijana katika kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu na kuwawezesha kuendelea kukisoma na kukihifadhi”.
Almayali ametoa shukrani za dhati kwa waliosaidia kufanikisha semina hizo, kuanzia muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mkoa huo, wakufunzi wa semina na viongozi wa huseiniyya na misikiti iliyotumika kuendeshea semina”.
Mahafali imepambwa na vitu vingi, ukiwemo wimbo wa (Ashbaalil-Kafeel), uliobeba kaulimbiu ya mwaka huu 2023 chini ya muimbaji Muhammad Baaqir Qahtwani, huku kikosi cha Ahbaabu-Zaharaa (a.s) kikiwa na ushiriki mkubwa, mahafali ikahitimishwa kwa kugawa zawadi kwa watu waliosaidia kufanikisha mradi huo.