Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imewapa mitihani ya nadhariyya na vitendo walimu wa malezi ya kiislamu katika mji wa Najafu kupitia program ya kujenga uwezo awamu ya tatu.
Semina inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.
Maswali ya mtihani yamehusisha somo la hukumu za usomaji wa Qur’ani, kusimama, kuanza, maandishi ya msahafu, sauti, naghmah, Aqida katika Qur’ani, njia za kuhifadhi Qur’ani, njia za ufundishaji na elimu ya jamii.
Semina hii ni sehemu ya ratiba ya masomo ya Qur’ani katika mkoa wa Najafu, iliyo andaliwa na Maahadi mwaka 2023 kwa lengo la kueneza usomaji wa Qur’ani katika jamii.