Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inaendelea na vikao vya usomaji wa Qur’ani vya kila wiki (Arshu-Tilawah) katika jengo la Alqami.
Vikao hivyo vinasimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Katika ujumbe uliotolewa na Ahmadi Najafi kwa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji, kuhusu umuhimu wa kupambika na mafundisho ya Qur’ani katika Maisha ya watu sambamba na umuhimu wa kufanya tafakuri.
Hafla imepambwa na kisomo cha Sajjaad Soledri kutoka Iran na Sayyid Hussein Khurasani.
Huku wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wakisoma kwa vikundi, na kikosi cha Nuur kikasoma tenzi za kidini.