Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, inafanya shindano la Alfurqaan la kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu awamu ya sita katika mji wa Najafu.
Kiongozi wa Maahadi bibi Manara Aljaburi amesema “Katika awamu ya kwanza ya shindano hilo Maahadi imepokea washiriki (50) waliohifadhi Qur’ani tukufu kutoka mkoa wa Najafu”.
Akaongeza kuwa “Shindano limefunguliwa kwa aya za Qur’ani tukufu, kisha kamati inayosimamia shindano hilo ikatoa maelekezo, halafu shindano likaanza”.