Atabatu Abbasiyya imepokea maelfu ya mazuwaru katika mazingira yaliyojaa huzuni.

Mazingira ya huzuni yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu, karibia na shughuli ya kubadili bendera ya kubba la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kama ishara ya kuanza kwa mwezi wa Muharam.

Atabatu Abbasiyya imepandisha bendera zinazoashiria huzuni katika ukumbi wa haram tukufu na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili kama ishara ya kuupokea mwezi wa Muharam na Safar.

Siku ya Jumanne Atabatu Abbasiyya imepokea maelfu ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, wanaokuja kushiriki kwenye shughuli ya kubadili bendera za malalo mawili matakatifu.

Atabatu Abbasiyya itabadilisha bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya swala ya Magharibi na Ishaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: