Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amesema kuwa, kufanya maombolezo ya Ashura ni kuhuisha uimamu, waumini wanatakiwa kutilia umuhimu swala hilo na kushiriki.
Ameyasema hayo katika shughuli ya kubadili bendera ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kutoa bendera nyekundu na kuweka nyeusi, iliyofanywa katika uwanja wa mbele ya mlango wa Kibla.
Sayyid Swafi amesema kuwa “Kujiandaa kinafsi na kuonyesha mazingira ya huzuni kwa kuvaa nguo nyeusi ni utamaduni muhimu kwa waislamu wa dunia nzima, wakati wanapo omboleza Ashura ambayo ni sawa na kuhuisha uimamu”, ametoa wito kwa waumini “washiriki kwenye maomboleza hayo kama walivyo husia Maimamu (a.s), kutilia umuhimu na kushiriki maombolezo haya ni jambo tukufu”.
Akaongeza kuwa “Maombolezo ya Ashura yanatakiwa kufanywa kwa njia maarufu ambazo hutumika kuonyesha huzuni na majonzi”.
Kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi amesisitiza “Ulazima wa kuomboleza Ashura kwa kutumia njia zinazo endana na msiba unaoumiza nyoyo za waumini”.
Akasema kuwa “Hakika tukio la Twafu linamafundisho mengi kutokana na jinai zilizofanywa na waovu wa umma huu”.
Akaendelea kusisitiza kuwa historia ya Iraq ilijirudia kwa kutokea vitendo vya kigaidi katika miaka ya hivi karibuni, “Shetani alishawishi wafuasi wake kuuwa waumini”, Hakika mauwaji mabaya ya wanaume kwa wasichana na watoto yaliyofanywa katika taifa la Iraq hakuna anaejua mwisho wake ispokua Mwenyezi Mungu mtukufu, kama sio huruma ya Mwenyezi Mungu kupitia Marjaa-Dini mkuu Sayyid Sistani kwa kutoa fatwa takatifu iliyolinda taifa na maeneo matukufu, shukrani za pekee ziende kwa walioitikia fatwa yake, wakajitolea kunusuru haki dhidi ya batili.