Chuo kikuu cha Al-Ameed kimeweka mapambo yanayoashiria huzuni katika lango la chuo, kufuatia kuingia kwa maombolezo ya kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuari wake katika siku ya Ashura.
Kamati ya mapambo imeweka mabango na bendera nyeusi kwa ajili ya kuomboleza kifo cha baba wa watu huru Imamu Hussein (a.s), aliyeuwawa kwa ajili ya kutetea uhuru na utukufu wa mwanaadamu.
Maeneo yote ya chuo yamewekwa mapambo meusi, kufuatia kuingia mwezi wa huzuni mwezi wa Muharam.
Chuo kikuu cha Al-Ameed huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s), ikiwa ni sehemu ya kufuata mafundisho ya Imamu Swadiq (a.s) yanayo himiza kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s).