Bendera ya huzuni za Ashura imepandishwa kwenye majengo ya Abbasi (a.s) ya makazi kama ishara ya kuonyesha kuingia kwa mwezi wa huzuni.

Imepandishwa bendera ya huzuni za Ashura kwenye majengo ya Abbasi (a.s) ya makazi chini ya Atabatu Abbasiyya kama ishara ya kuingia kwa mwezi wa Muharam 1445h.

Kiongozi wa majengo hayo Sayyid Haidari Majhuul Muhammad amesema “Tumefanya halfa ya kupandisha bendera inayoashiria kuanza kwa huzuni za Ashura iliyohudhuriwa na idadi kubwa ya wakazi wa nyumba hizi, katika hafla hiyo imesisitizwa kuendelea na maombolezo ya Imamu Hussein (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Watumishi wa Majengo hayo wameanza kutekeleza ratiba maalum ya kuomboleza yenye vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na kuweka mabango sehemu mbalimbali za majengo hayo, kufanya majlisi za kuomboleza sambamba na kutoa huduma mbalimbali kwa waombolezaji”.

Vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya tukufu, vinafanya juhudi kubwa ya kutoa huduma bora kwa waombolezaji na mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: