Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake inafanya kikao cha usomaji wa Qur’ani kufuatia kuingia kwa mwezi wa Muharam.

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya kikao cha usomaji wa Qur’ani kufuatia kuingia kwa mwezi wa Muharam na kuomboleza tukio la Karbala.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema “Tukio la Karbala ni jambo kubwa wa waumini, kutokana na yaliyojiri kwa Ahlulbait (a.s) na kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s), tumefanya kikao cha usomaji wa Qur’ani tukufu”.

Akaongeza kuwa “Kikao hicho kimepambwa na muhadhara wenye anuani isemayo (Kuhuisha nafsi kwa kukumbuka mapinduzi ya Islahi), yameelezwa masomo na mazingatio yanayopatikana kutokana na msimamo wa Imamu Hussein na bibi Zainabu (a.s) na umuhimu wa kufuata mwenendo wao, sambamba na kufafanua baadhi ya maelekezo ya kiroho, kimaadili na kidini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: