Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya nadwa mjini Mombasa kusini mwa nchi ya Kenya katika bara la Afrika.
Nadwa hiyo imesimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo.
Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Nadwa imefanywa kwa hushirikiana na muhubiri wa Markazi Shekhe Yunus Issa, imedumu kwa muda wa siku mbili, siku ya kwanza ilihusu wanawake na siku ya pili wanaume, imehudhuriwa na makumi ya wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Mihadhara iliyotolewa imejikita katika kueleza mafundisho halisi ya Dini tukufu ya kiislamu ya kimaadili na kiimani, aidha imefafanuliwa athari ya mafundisho hayo katika kila zama, sambamba na kuhimiza kusoma Dini na kufahamu misingi na matawi yake pamoja na vitendo vya kila siku”.
Akasisitiza kuwa “Markazi inaendelea kufanya nadwa na ratiba zingine za kitablighi katika nchi tofauti za Afrika”, akasema “Kuna mihadhara mingi na nadwa zitakazo fanywa wakati wa mwezi huu mtukufu wa Muharam, katika kuomboleza kifo cha bwana wa mashahidi (a.s)”.