Wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani wanashiriki kwenye jaribio linaloendeshwa na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya kwa lengo la kuboresha vipaji vyao.
Idara ya Tahfiidh chini ya Maahadi ya Qur’ani ndio waandaaji wa jaribio hilo.
Jaribio limefanywa mjini Karbala na linawashiriki kutoka Baghdad na Baabil, lengo ni kuangalia uwezo wao katika hifdhu, na kuendeleza harakati za Maahadi katika kuhifadhisha Qur’ani tukufu.
Idara huandaa semina mbalimbali za kuhifadhisha Qur’ani tukufu na kutoa wahitimu wa juzu tofauti za Qur’ani.