Kitengo cha utumishi kinatumia maeneo mapya katika kuhifadhi mabegi ya mazuwaru na mali zao.

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya kimetengeneza maeneo mapya ya kuhifadhia mabegi ya mazuwari na mali zao katika siku za Ashura.

Kiongozi wa idara ya Amanaat chini ya kitengo hicho Sayyid Jafari Aali Twa’amah amesema “Idara imeongeza maeneo ya kutunzia mabegi ya mazuwaru”.

Akaongeza kuwa “Idara imeandaa sehemu mpya ya kuweka viti-mwendo vya watu wenye ulemavu na watoto upande wa mlango wa Baghdad, akasema kuwa kabati moja lilikuwa na namba zaidi ya (500) zimeongezwa na kuwa zaidi ya (1000) kwa ajili ya kurahisisha upokeaji na utunzaji wa mali za mazuwaru”.

Vitengo vya Atabatu Abbasiyya vinafanya kazi kubwa ya kuhakikisha vinatoa huduma bora kwa mazuwaru wanaokuja kufanya ziara ya Ashura kutoka ndani na nje ya taifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: