Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza utaratibu wa kugawa maji ya kunywa kwa mazuwaru wa Ashura.
Kiongozi wa idara ya maji Sayyid Naiim Abudi amesema “Utaratibu maalum wa kugawa maji unahusisha gari za maji (15) kila siku, kila moja inasanduku (1400) za maji, husambazwa kwa mawakibu zilizopo upande wa mlango wa Bagdad, Alqami, Kibla, Hauraa hadi kwenye mlango wa Imamu Ali (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Tutaandaa maji na kuweka barafu kwa ajili ya kugawa kwenye matembezi ya Towareji mwezi kumi Muharam, katika maeneo ya karibu na malalo tukufu”.
Kwa mujibu wa maelezo ya Abudi amesema kuwa “Idara inagawa vipande (5000) vya barafu kila siku kwenye mawakibu zilizopo katika maeneo tuliyotaja, husambazwa kwa kutumia gari maalum, sambamba na kuweka barafu kwenye mahodhi ya maji yanayozunguka eneo la Ataba tukufu”.