Mmoja wa mahafidh wa Maahadi ya Qur’ani idara ya wanawake amepata nafasi ya juu kwenye mashindano ya mimbari za nuru.

Bi Nuru Sataar Khalili mmoja wa wanafunzi wa Maahadi ya Qur’ani idara ya wanawake/ tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya amekuwa mshindi wa tatu kwenye shindano la mimbari za nuru la kuhifadhi Qur’ani tukufu.

Shindano limesimamiwa na Madrasa ya Fatuma binti Asadi (a.s), chini ya idara ya shule za Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya.

Mkuu wa Maahadi Bibi Nida Abdusataar amesema “Ushindi wa mwanafunzi wa Maahadi ni Fahari kwake na rafiki zake kunawatia moyo wa kuendelea kuhifadhi Qur’ani tukufu”.

Akaongeza kuwa “Bi Nuru amekuwa mshindi wa tatu kwenye shindano la mimbari za nuru la kikundi cha waliohifadhi juzu tano za Qur’ani”, akabainisha kuwa “Bado anaendelea kuhifadhi hadi amalize msahafu wote tena kwa usomaji mzuri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: