Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeandaa ratiba ya ushiriki wa wasomaji wake kwenye majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) kila siku.
Mkuu wa kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa Sayyid Hasanaini Halo amesema “Walimu na wanafunzi wa mradi wa Qur’ani, wamesambazwa kwenye Majlisi-Husseiniyya za asubuhi na jioni zinazofanyika ndani na nje ya Ataba tukufu”.
Akasema kuwa “Kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani kwenye majlisi za kuomboleza ni ratiba ya lazima kwenye majlisi tofauti, aidha ni jambo muhimu katika kutumikia vizito viwili”, akaongeza kuwa “Ni jambo zuri kutumia kipindi cha Muharam kueneza utamaduni wa kusikiliza Qur’ani tukufu”.
Akaendelea kusema: “Atabatu Abbasiyya ni miongoni mwa taasisi za mwanzo kuwa na utaratibu huo, hakika usomaji wa Qur’ani tukufu hutoa ujumbe muhimu kwenye majlisi za Husseiniyya.