Uwanja mtukufu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa siku ya nne mfululizo, umeendelea kushuhudia majlisi za kuomboleza za wanawake, kufuatia tukio la Ashura.
Majlisi hizo zinasimamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya na kuhudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru na waombolezaji.
Mhadhiri wa mimbari Husseiniyya kutoka kitengo cha Dini Shekhe Ali Mujani ameongea kuhusu madhumuni ya ziara ya Ashura, ambayo huangazia uhusiano baina ya waumini na Imamu Hussein (a.s) sambamba na faida zake.
Majlisi zinafanywa katika kumi la kwanza la mwezi wa Muharam, ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), zitahitimishwa siku ya mwezi tisa muharam.
Uongozi mkuu unatoa kipaombele cha kufanya majlisi za kuomboleza matukio ya kuuwawa kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), hupewa umuhimu wa pekee siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Muharam, siku ambazo aliuwawa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake.