Katika nchi ya Naijeria.. Kitengo cha Habari na utamaduni kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s).

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s) katika nchi ya Naijeria, mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Shimri amesema “Markazi imefanya majlisi ya kuomboleza katika mji wa Nasrawi nchini Naijeria, iliyo hutubiwa na Shekhe Muhammad Abdallah Twaibu, ameongea kuhusu tukio la Ashura lililomkumba Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake, Shekhe Muhammad Abdallah Twaibu amebainisha namna Imamu Hussein (a.s) alivyojitolea kwa ajili ya kulinda Dini ya Uislamu na akaeleza wajibu wa kila muislamu na mpenzi wa Ahlulbait (a.s)”.

Kwa mujibu wa maneno ya mkuu wa Markazi, “Majaalisi za Ashura zinafanywa kwenye nchi tofauti za Afrika chini ya usimamizi wa mubalighina wa Markazi, wanabainisha mapinduzi ya Imamu Hussein na athari yake kwa mwanaadamu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: