Lango la mji mkongwe na Barabara zinazoelekea kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), zimeshuhudia mawakibu za waombolezaji katika siku ya mwezi tano Muharam.
Mawakibu za uombolezaji leo zimewakumbuka wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) waliojitolea kwa ajili yake (a.s) kwa kueleza msimamo wao wakati wa vita ya Twafu, huku wakiimba qaswida na tenzi za kuomboleza zilizo amsha hisia za majonzi na huzuni.
Siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Muharam ni maalum kwa mawakibu za watu wa Karbala, huo ndio utamaduni wa miaka mingi katika uombolezaji wa mwezi wa Muharam, mawakibu za (zanjiil) na (matam) hujitokeza kwa wingi kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s).
Harakati za mawakibu zinafata ratiba maalum iliyoandaliwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya, zinatembea kwa kutumia barabara zilizopangwa hadi kwenye mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha huingia ndani ya ukumbi wa haram hiyo na kutokea mlango wa Imamu Hussein (a.s) na kuelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) kwa kupita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Kunakikosi cha watumishi wa kitengo ambacho hufuatana na mawakibu kuanzia mwanzo wa matembezi yao hadi mwisho, kwa ajili ya kulinda usitokee muingiliano baina ya mawakibu na mazuwaru.