Maahadi ya Qur’ani idara ya wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea na shindano la kuhifadhi Qur’ani tukufu kwa wanafunzi wa Najafu na Dhiqaar.
Kiongozi wa Maahadi Bibi Manaar Aljaburi amesema “Uongozi wa Maahadi imefanya kikao maalum cha kuhitimisha shindano la Qur’ani awamu ya sita lililoanza wiki iliyopita”.
Akaongeza kuwa “Washiriki wa shindano hili walikuwa (150) kutoka mikoa tofauti ya Iraq”, akasema: “Shindano lilikuwa na makundi matatu ambayo ni (waliohifadhi juzuu 15, 20 na 30)”.
Akabainisha kuwa “Washindi wa shindano hili watapata nafasi ya kushiriki kwenye shindano kubwa la kitaifa linalotarajiwa kufwanywa katika mwezi wa Rabiul-Awwal”.