Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya idara ya wanawake, kinatoa mihadhara yenye anuani isemayo (Haki za ulimi na changamoto zake kwa mtazamo wa Risalatul-Huquqi ya Imamu Zainul-Aabidina (a.s) na namna ya kufanyia kazi).
Muhadhara umefanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Ashura ni fursa ya kurekebisha maadili na familia) ikiwa ni sehemu ya majlisi za kila siku, mhadhiri ni Nabaa Swabahu Alhaidari, ameongea kuhusu lugha za kimaadili na athari zake kijamii, kifamilia na kinafsi.
Kituo cha utamaduni wa familia kinatangaza utamaduni wa Ahlulbait (a.s) kwa ajili ya kuweka utulivu katika familia jamii na nafsi.
Kituo kinaendelea kutoa mihadhara kwa jamii ya wanawawake ndani ya mwezi huu wa Muharam sambamba na kueleza yaliyotokea katika historia hususan tukio la Twafu, kwa ajili ya kupata mazingatio na kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s).