Kwa picha.. Kuendelea kumiminika mawakibu za kuomboleza jioni ya mwezi sita Muharam.

Mawakibu za kuomboleza zinaendelea kumiminika katika Atabatu Abbasiyya tukufu, jioni ya siku ya sita ya mwezi wa Muharam kwa ajili ya kuhuisha maombolezo ya kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake.

Njia zinazo elekea kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zimejaa mawakibu za waombolezaji.

Mawakibu nyingi za (zanjiil) zimewasili jioni ya leo siku ya Jumanne mwezi sita Muharam kama ilivyo testuri ya mawakibu hizo kila mwaka.

Siku kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam ni maalum kwa mawakibu za watu wa Karbala za matam na zainjiil.

Matembezi ya mawakibu yanafanyika kwa kufuata utaratibu uliowekwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, hutembea katika Barabara maalum zinazoelekea kwenye mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hadi kwenye ukumbi wa haram yake na kutokea mlango wa Imamu Hussein (a.s) hadi kwenye malalo ya Bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) kwa kupitia uwanja wa katikati ya haram mbili.

Kitengo kimeweka watumishi maalum wanaofuatana na kila maukibu kuanzia mwanzo wa matembezi yake hadi mwisho, sambamba na kuzingatia utulivu na kujiepusha na msongamano kati ya mawakibu na mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: