Baada ya barua ya Sayyid Sistani.. Umoja wa mataifa umepitisha azimio la kufanya mazungumzo baina ya Dini.

Baada ya barua ya Marjaa Dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Sistani kuhusu tukio la kuchoma msahafu mtukufu nchini Swiden, umoja wa mataifa umepitisha azimio la kufanya mazungumzo baina ya Dini na tamaduni tofauti, na kupinga khutuba za kujenga chiki.

Marjaa Dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Sistani aliandika barua ya kulaani tukio la kuchomwa Qur’ani tukufu huko nchini Swiden, akautaka umoja wa mataifa uchukue hatua za kuzuwia jambo hilo lisijirudie tena.

Kwa mujibu wa tamko la katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres, amethibitisha kupokea barua ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, na amefuatilia tukio hilo na hasira za waislamu wa Iraq na dunia nzima, amesema kuwa haungi mkono uchomwaji wa Qur’ani na analaani vikali kitendo hicho kiovu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: