Katika matembezi ya kuomboleza.. Mawakibu-Husseiniyya zinainua misahafu mitukufu.

Mawakibu za kuomboleza zimeinua misahafu kwenye matembezi ya uombolezaji wa Husseiniyya katika mwezi wa Muharam, kama ishara ya kuonyesha kushikamana kwao na Qur’ani tukufu na kulaani kufanyiwa uwadui kitabu hicho kitakatifu.

Rais wa maadhimisho na Mawakibu Husseiniyya Sayyid Aqiil Yasiri amesema “Katika matembezi ya kuomboleza mwaka huu katika mji wa Karbala, Mawakibu zimenyanyua misahafu na bendera ya Iraq kama ishara ya kuonyesha mapenzi yao kwa Qur’ani tukufu, kitabu ambacho ni rehema kwa walimwengu wote kunacho fundisha amani na kuvumiliana baina ya watu”.

Akaongeza kuwa “Kunyanyua Qur’ani tukufu ni ishara ya kulaani vitendo vya watu waovu wanaodhalilisha kitabu hicho kitakatifu, na kunyanyua bendera ya Iraq ni ishara kuwa raia wa Iraq wanaipenda Qur’ani na wameshikamana nayo”.

Akasisitiza kuwa “Mawakibu za kuomboleza zinaendelea kumiminika ndani ya siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Muharam, matembezi yanafanywa kwa utaratibu mzuri kuanzia asubuhi hadi usiku kwa kufuata ratiba maalum”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: