Kitengo cha malezi na elimu kinafanya majlisi ya kuomboleza katika siku ya mwezi saba Muharam.

Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kimefanya majlisi ya kuomboleza mwezi saba Muharam.

Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Haidari Husseini A’raji amesema “Kitengo hufanya majlisi ya kuomboleza kila mwaka siku ya mwezi saba Muharam, katika kukumbuka yaliyojiri siku hiyo na kuuwawa kishahidi kwa mwezi wa Bani-Hashim (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Majlisi imepambwa na mawaidha yaliyojikita katika mafunzo ya kimaadili na utukufu wa kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s) sambamba na kufafanua maana za jina la mwezi wa familia na kwa nini alipewa jina hilo wakati ambao familia ilikuwa na watakasifu (maasumina) watatu”.

Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma qaswida na tenzi za kuomboleza, zilizo elezea kifo cha Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuamsha hisia za huzuni na majonzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: