Maahadi ya Qur’ani idara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imeomboleza kifo cha Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kufanya majlisi ya uombolezaji katika siku ya mwezi saba Muharam.
Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema “Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu ukafuata muhadhara kuhusu historia ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na utukufu wake”.
Akaongeza kuwa “Majlisi imepambwa na tenzi za kuomboleza, zilizotaja mazingira ya mwezi saba Muharam katika jangwa la Twafu na kuhitimisha kwa kusoma dua”.
Atabatu Abbasiyya kupitia vitengo vyake vyote vya ndani na nje ya mji wa Karbala, imeandaa ratiba za uombolezaji na utoaji wa huduma kufuatia msiba wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) sambamba na kukumbuka namna watu wa nyumba ya Mtume (a.s) walivyo jitolea.