Miongoni mwake ziara kwa niaba.. majukumu tofauti yanafanywa na idara ya Masayyid kwa mazuwaru wa Ashura.

Idara ya Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya inamajukumu mengi kwa mazuwaru wa Ashura.

Mmoja wa wahudumu wa idara hiyo Sayyid Muhammad Swalehe amesema “Idara inamajukumu mengi, ikiwemo ziara kwa niaba, kwa waliojisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba uliopo kwenye mtandao wa Alkafeel pamoja na swala ya rakaa mbili, kwa wale walioshindwa kuja Karbala kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Wahudumu wa idara hii wapo kazini siku zote za mwezi mtukufu wa Muharam, miongoni mwa kazi wanazofanya ni kusafisha dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s), milango, kabati za vitabu, kupuliza marashi, kugawa vitabu vya ziara, kufanya ziara pamoja na jeneza, kupokea wageni wanaoingia Ataba na kuwasomea ziara”.

Akaendelea kusema, watumishi wa idara ya Masayyid kwa kushirikiana na idara ya zawadi na nadhiri, huchukua vitambaa (vilivyo wekwa au kufungwa) kwenye dirisha takatifu na kuvigawa kwa mazuwaru wanahitaji kukidhiwa haja zao na kufanyiwa wepeshi mambo yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: