Wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, wamemaliza kazi ya kutandika zulia lekundu katika eneo lote linalozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Abbasi Ali Abu Aufu amesema “Wahudumu wa kitengo chetu wamemaliza kazi ya kutandika zulia lekundu katika eneo lote linalozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama sehemu ya kujiandaa na ziara ya mwezi kumi Muharam na matembezi ya Towareji”.
Kuhusu utunzaji wa mali za mazuwaru amesema: “Kutokana na kuongezeka idadi ya mazuwaru, kitengo kimeongeza maeneo matatu ya kupokea mabegi ya mazuwaru na mali zao, sambamba na kufanya upanuzi katika maeneo mengine”.
Kitengo cha utumishi kinafanya juhudi kubwa ya kuhakikisha kinatoa huduma bora kwa mazuwaru wanaokuja kufanya ziara ya Ashura kutoka ndani na nje ya nchi.