Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimekutana na viongozi wa idara ya elimu na wanafunzi wa Dini katika jimbo la Kaduna nchini Naijeria.
Kitengo kimewakilishwa na wajumbe kutoka Markazi Dirasaati Afriqiyya ambao ni wawakilishi wa Markazi wa nchini Naijeria, nao ni Shekhe Shamsu-Dini Abdullahi na Shekhe Ibrahim Mussa.
Shekhe Abdullahi amesema: “Kutembelea shule za Dini ni sehemu ya kudumisha mawasiliano na taasisi za Dini, tumekutana na viongozi wa idara za elimu na wanafunzi sambamba na kuangalia mfumbo wa masomo”.
Akaongeza kuwa “Msingi wa kusoma ni kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu na kutambua Dini sahihi chini ya mwenendo wa Ahlulbait (a.s) kwani wao ndio walimu wa uislamu halisi Almuhammadiyya”.
Muwakilishi wa Markazi amesema kuwa “Tulipata nafasi ya kutoa nasaha kwa wanafunzi, tukasisitiza umoja na undugu katika safari ya kutafunta elimu ya Dini”.