Watoto wamekuwa na nafasi maalum katika majlisi za kuomboleza zinazofanywa na wahadhiri wa Husseiniyya idara ya wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika maombolezo ya Ashura.
Idara inaendelea na majilisi za kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na familia yake (a.s) zinazo hudhuriwa na idadi kubwa ya wakinamama na watoto.
Idara inatumia ushiriki wa watoto kutoa malezi mema yanayofuata misingi ya Ahlulbait (a.s).
Ushiriki wa watoto kwenye majlisi za Husseiniyya umekuwa jambo la kawaida na linasaidia kufikisha ujumbe wa Imamu Hussein (a.s) kwa vijana na mabinti.