Huzuni na majonzi vimetanda katika mji wa Karbala kwenye maombolezo ya Ashura.

Huzuni na majonzi vimetanda katika mji wa Karbala wakati huu wa kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) kilichotokea siku ya Ashura.

Kundi kubwa la waumini kutoka ndani na nje ya mji wa Karbala linashiriki katika maombolezo hayo mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Atabatu Abbasiyya imejipanga vizuri kutoa huduma kwa waombolezaji na mawakibu Husseiniyya zilizopo kwenye Barabara tofauti zinazoelekea katika haram mbili tukufu, huku maandalizi ya matembezi ya Towareji yakiwa yamekamilika, matembezi hayo yataanza baada ya swala ya Dhuhurain ya leo.

Mamilioni ya waombolezaji kutoka ndani na nje ya Iraq huja kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na familia yake (a.s) pamoja na wafuasi wake siku ya mwezi kumi Muharam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: