Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ameswalisha sawala ya Dhuhurain katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Swala ya Dhuhurain ya siku ya mwezi kumi Muharam, imehudhuriwa na kundi kubwa la waombolezaji wa kifo cha Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake kilicho tokea siku kama hiyo.
Huzuni na majonzi vimetanda katika nyoyo za waombolezaji wakikumbuka swala ya mwisho ya Imamu Hussein (a.s) kabla ya kuuwawa kwake.
Baada ya swala hiyo mji umeshuhudia kundi kubwa la waombolezaji wanaoshiriki matembezi ya Towareji.