Matembezi yalianzia katika eneo la kituo cha Salaam, kilichopo umbali wa kilometa nne kutoka haram ya Imamu Hussein (a.s), wakapita barabara ya Jamhuriyya hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s), wakapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na kuingia kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) huku ulinzi na usalama ukiwa umeimarishwa na Ataba tukufu.
Atabatu Abbasiyya imeandaa milango minne ya kuingilia washiriki wa matembezi ya Towareji, na milango mitano ya kutokea.