Jioni ya leo kundi kubwa la waumini limekuja kuomboleza usiku wa kumi na moja Muharam, na kukumbuka yaliyojiri kwa Imamu Hussein (a.s) baada ya kuisha vita ya Twafu.
Waumini wa Karbala wamezowea kufanya maombolezo hayo katika usiku wa kumi na moja Muharam, ujulikanao kama “usiku wa wahsha”, ambapo hukumbuka yaliyojiri kwa mateka wa Imamu Hussein (a.s).
Waombolezaji huja moja kwa moja katika malalo ya mnyweshaji wenye kiu Karbala Abulfadhil Abbasi (a.s) kumpa pole kisha huelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s).
Maombolezo hayo hujumuisha usomaji wa tenzi na qaswida za kuomboleza, kuwasha mishumaa katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na jirani ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya.