Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika kuomboleza Ashura kwa ushiriki wa mazuwaru wa bwana wa mashahidi (a.s).
Idara ya Tahfiidh imehuisha usiku huu mtukufu katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) “Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa Shekhe Jawadi Nasrawi amesema, tumesoma Qur’ani tukufu kwa ushiriki wa mazuwaru na kuelekeza thawabu zake kwa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake”.
Akaongeza kuwa “Jambo hili ni sehemu ya kufuata mwenendo wa bwana wa mashahidi (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake, waliokesha usiku kama huu kwa kumtaja Mwenyezi Mungu, tumepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru watukufu”.
Imekuwa desturi ya Maahadi ya Qur’ani kuhuisha siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Muharam kwa kusoma Qur’ani tukufu, kwa ushiriki wa wafuasi wa Ahlulbait (a.s).