Hivi karibuni Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imechapisha jarida la Riyadhu-Zaharaa (a.s) namba (196), ambalo hutolewa kila mwezi.
Hilo ni jarida la kwanza kutolewa na Ataba za Iraq tangu mwaka (2003m).
Toleo jipwa linamambo mengi kwenye sekta tofauti, ikiwa ni pamoja na Fiqhi, Aqida, Qur’ani, Malezi, Elimu, Utamaduni, Jamii, Afya pamoja na mambo mengine.
Kuna anuani tofauti za mada kwenye toleo hili, miongoni mwa anuani hizo ni (Haki za Maasumina (a.s) - Sauti ya kulia – Salam kwa Sayyid Zamaan – Firdausi nae neo lake la kijani – Mwanamke alikuwa na ushiriki kwenye shughuli za wiki ya Imamu kimataifa – Kuhisi upweke – matokeo ya teknolojia za kisasa, kuna eneo maalum lina mada tofauti kuhusu Ashura.