Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kinafanya Majlisi za kuomboleza kumbukumbu ya Ashura katika maeneo tofauti ya mkoa wa Nainawa.
Kiongozi wa idara ya maelekezo na msaada chini ya kitengo cha Shekhe Haidari Aaridhwi amesema “Majlisi za kuomboleza zinafanywa chini ya maelekezo ya Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi kwenye maeneo tofauti hapa mkoani, miongoni mwa maeneo hayo ni Sahal-Nainawa, Kubba, wilaya ya Shaikhani na Sanjaar”.
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imekuwa ikifanya Majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na familia yake (a.s), sambamba na kutoa huduma mbalimbali kwa waombolezaji na kuweka mazingira ya huzuni”.
Akabainisha kuwa “Majlisi zimepambwa na mihadhara ya kidini kuhusu tukio la Ashura na dhulma alizofanyiwa Imamu Hussein (a.s) katika Maisha yake”, tambua kuwa Majlisi hizo zitahitimishwa mwezi kumi na tatu Muharam.