Kuhitimisha matembezi ya kuomboleza maziko ya miili mitakatifu katika siku ya mwezi kumi na tatu Muharam.

Siku ya mwezi kumi na tatu Muharam kabila la bani Asadi limehitimisha matembezi yao katika mji wa Karbala, ambayo huchukuliwa kuwa ya pili kwa ukubwa baada ya matembezi ya Towareji, waombolezaji wameingia katika Ataba mbili tukufu kuomboleza maziko ya mashahidi wa Karbala kwa utaratibu mzuri.

Jumla ya maukibu mia moja na ishirini kutoka mkoa wa Karbala zimeshiriki kwenye maombolezo ya kumbukumbu ya kuzikwa mashahidi wa Karbala, pamoja na wageni kutoka maeneo mengine, matembezi hayo yamehitimishwa kwa waombolezaji wote kuingia katika Ataba mbili tukufu, nayo ndio matembezi makubwa baada ya matembezi ya Towareji.

Kabila na koo mbalimbali za raia wa Iraq zimeingia katika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya kuomboleza, wamejikumbusha yaliyojiri katika ardhi ya Karbala mwaka 61h, kabila la bani Asadi liliposhirikiana na Imamu Sajaad (a.s) kuzika miili ya mashahidi kama riwaya zinavyo sema, kuanzia wakati huo siku ya mwezi kumi na tatu Muharam imekuwa siku maalum ya kuomboleza tukio hilo.

Imeshuhudiwa idadi kubwa ya wanawake waliotoka kumpa pole bibi Zainabu (a.s) kutokana na msiba huo mkubwa.

Atabatu Abbasiyya imejipanga kutoa huduma bora kwa mawakibu za waombolezaji na kuratibu matembezi katika utaratibu mzuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: