Majmaa-Ilmi inaendelea kufanya Majlisi za kuomboleza tukio la Twafu.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kwa siku ya pili mfululizo imeendelea kufanya Majlisi za kuomboleza mashahidi wa Karbala.

Majlisi inafanywa kwa wanafunzi wa tahfiidh katika Maahadi ya Qur’ani mjini Najafu chini ya Majmaa.

Majlisi za kuomboleza ni sehemu ya harakati za Maahadi zinazolenga kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani tukufu katika vikao vya husseiniyya.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na Muhammad Ridhwa, ikafuatiwa na qaswida ya kuomboleza iliyosomwa na wanafunzi wa kuhifadhi Qur’ani mbele ya wazazi na viongozi wa Maahadi ya Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: