Watumishi wa Atabatu Abbasiyya wanasafisha milango ya haram takatifu.

Watumishi wa Atabatu Abbasiyya wanasafisha minago ya haram takatifu, baada ya kumaliza msimu wa ziara ya Ashura.

Makamo rais wa kitengo cha kulinda nidham Sayyid Ridhwa Naji Sahi amesema “Kwa kushirikiana na vitengo vya haram tukufu na wahudumu wa kujitolea, tunasafisha milango yote ya haram baada kumaliza ziara ya Ashura na matembezi ya Towareji”.

Akaongeza kuwa: “Mwanzoni mwa mwezi wa Muharam tuliweka mchanga kwenye minago ya haram kwa ajili ya kuzuwia mazuwaru wasianguke kwenye milango hiyo wakati wa kufanya ziara tukufu, hususan katika matembezi ya Towareji”.

Akabainisha kuwa “Wahudumu wa kujitolea kutoka Karbala walileta michanga na kuweka kwenye milango ya Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na wahudumu wa Ataba, wamekuwa wakifanya hivyo kwa miaka 19 sasa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: