Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imehitimisha Majlisi za kuomboleza tukio la Twafu.
Majlisi imehusisha wanafunzi wanaohifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu katika Maahadi ya Qur’ani tukufu mjini Najafu chini ya Majmaa.
Majlisi imefanywa siku tatu mfululizo, kwa lengo la kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani tukufu.
Majlis imepambwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Hassan Hadaad, shairi kutoka kwa Muhammad Ridhwa na muhadhara kutoka kwa Shekhe Qudama Khadhari, uliofuatiwa na qaswida ya uombolezaji kutoka kwa Abbasi Naswari, mbele ya wazazi na viongozi wa Maahadi.
Katika Majlisi hiyo limeonyeshwa igizo lenye anuani isemayo (Tabswirah) lilifanywa na wanafunzi wa Maahadi, limeonyesha umuhimu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu katika kujenga Maisha yenye amani na upendo, yasiyokuwa na chuku wala uadui kama inavyo shuhudiwa katika zama hizi, likasisitiza umuhimu wa kusoma Qur’ani kwa mazingatio kama tulivyo husiwa na Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s).