Sayyid Swafi amekutana na watumishi wa kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amekutana na watumishi wa kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya waliopata vyeti vya uandishi wa Habari.

Kikao hicho kimehudhuriwa na kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami, mjumbe wa kamati kuu Sayyid Liith Mussawi, Dokta Abbasi Dida Mussawi na rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nuris Dahani.

Sayyid Muhammad Amiri Tamimi kutoka kitengo cha Habari amesema “Atabatu Abbasiyya chini ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, inafanya kazi daima ya kuandaa watumishi wa kitengo cha Habari, kwa kuwapa nafasi ya kusoma na kuongeza ujuzi wao katika sekta ya Habari”.

Akaongeza kuwa “Semina ya Habari walioshiriki baadhi ya watumishi wa kitengo cha Habari imedumu kwa muda wa siku tano, kila siku wamesoma saa saba” akasema “Semina za kujenga uwezo zimetupa uzowefu mkubwa, utakao tuwezesha kufikisha ujumbe wa Atabatu Abbasiyya kwa weledi”.

Mkufunzi wa semina hiyo Sayyid Alaa Jawadi Kadhim ameshukuru Atabatu Abbasiyya kwa kumpa nafasi hiyo adhim, iliyo muwezesha kutoa mchango wake wa kielmu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: