Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya semina ya uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq.
Wakufunzi wa semina hiyo ni wahadhiri wa vyuo vya Udaktari, na washiriki ni wanafunzi wa vyuo vya Udaktari na Uuguzi vya hapa Iraq.
Semina imedumu kwa muda wa siku mbili na imefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Almujtaba (a.s), wamefundishwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na (BLS), namna ya kutoa msaada wa awali kabla ya kumpeleka muathirika kwenye kituo cha afya.
Wanasemina hao wanatarajiwa kutoa huduma wakati wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) wamefundishwa kwa nadhariyya na vitendo, na wamepongeza masomo waliyofundishwa.