Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeandaa safari ya Kwenda Iran kutembelea malalo takatifu kwa wanafunzi waliohifadhi kitabu kwa Mwenyezi Mungu.
Ziara hiyo inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.
Msafara unaongozwa na kiongozi wa idara ya tahfiidh Shekhe Kadhim Khuz’ali na muongozaji wa malezi Shekhe Jaabir Khaqani wakiwa na wanafunzi kumi na moja.
Msafara huo utaanza kutembelea malalo ya Bibi Fatuma Maasuma bint wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s) kisha watatembelea malalo zingine katika nchi hiyo.
Kumbuka kuwa Maahadi inafanya mambo mbalimbali kwa wanafunzi wake wapatao (125), kwa lengo la kukuza vipaji vyao, ikiwa ni pamoja na kuandaa safari za kidini ambazo huhamasisha sana wanafunzi na kuwafanya wazingatie zaidi masomo yao.