Mtafiti na mhakiki kutoka Baharain Shekhe Hassan bun Ali Aali-Saiid, amepongeza harakati za kitengo cha maarifa ya kiislsmu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Ameyasema hayo alipotembelea kituo cha turathi za Hilla.
Mkuu wa kituo Shekhe Swadiq Khawilidi amemuonyesha Shekhe Aali-Saiid harakati zinazofanywa na kituo na matokeo yake, ikiwa ni pamoja na vitabu wanavyo chapisha na tafiti wanazofanya.
Aidha wameongea kuhusu ushirikiano wa kielimu baina ya nchi mbili, na ukatolewa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi katika sekta hiyo, Shekhe Aali-Saiid amepongeza kazi nzuri inayofanywa na kituo cha turathi za Hilla.
Shekhe Hassan Aali-Saiid ameshukuru kituo cha turathi za Hilla kwa kumpa nafasi ya kuwatembelea na mapokezi mazuri aliyopewa.